“Kituo cha biashara cha Lake Amu kilichopendekezwa mpango wa matumizi ya ardhi ya 2023”.

Kufuatia uzinduzi wa Upangaji na Upimaji wa eneo la Lake Amu kama Kituo cha Kibiashara na Mstahiki Gavana Issa Timamy majuma kadhaa yaliyopita huko Mpeketoni, hii leo Waziri wa Ardhi Tashrifa Bakari akiwa ameandamana na timu ya washauri pamoja na maafisa wengine wakuu kutoka Idara yake, wameandaa kikao na kamati simamizi ya eneo hilo, na kuiwasilisha rasimu ya plani iliyopendekezwa ili kuitathmini na kutoa maoni yao.

Baada ya hapo, rasimu hiyo itawasilishwa kwa wananchi ili kupokea maoni kabla ya kutekelezwa kwa mpango huo.

-Mwisho-

Kwa maelezo zaidi wasiliaana na afisi ya mawasiliano kwa:- communications@lamu.go.ke