Sadani Kupata Hati Miliki

Mstahiki Gavana Issa Timamy Kupitia Idara ya Ardhi, anatazamiwa kuweka kumbukumbu ya kihistoria baada ya kufanyika kwa uzinduzi wa upangaji na upimaji wa Ardhi ya Sadani Lamu Mashariki.

Hii leo,Waziri wa Ardhi, Mipango ya miji na Maji Tashrifa Bakari, amekutana na wakulima wa Sadani, ili kuunda kamati itakaosaidia kusimamia shughuli hiyo.

Aidha, Waziri Tashrifa aliitambulisha kampuni ya Utaalamu wa kupima mashamba na kupanga miji ya B & L SURVSPACE LTD, iliyotekwa jukumu la kupima eneo hilo la Sadani kwa wananchi.

Eneo la Sadani lilikuwa ni makaazi na mashamba ya ukulima kabla ya wenyeji wake kuhama kufuatia uvamizi wa shifta.

Akizungumza na wakaazi hao, Waziri Tashrifa amewasihi wakaazi hao na hasa kamati iliyochaguliwa, kushirikiana na wataalamu wa upimaji pamoja na maafisa wa serekali ya Kaunti kufanikisha zoezi hilo.

Waliokuwepo ni Afisa mkuu wa Ardhi Ahmed Ali pamoja na Mkurugenzi wake Patrice Lumumba na Easter Nzai wa Tume ya Ardhi nchini (NLC)Lamu, miongoni mwa wengine.