Simambae kupata hati miliki baada ya miongo 6 ya mahame

Idara ya Ardhi imezindua rasmi upimaji wa Kijiji cha zamani cha Simambae kilichoachwa mahame kwa miongo 6 baada ya wakaazi wake kuhama kwa lazima kufuatia uvamizi Wa kinyama washifta.

Kijiji hicho cha zamani, kilivunjika baada ya watu wake kuhamia maeneo ya Malindi, Kilifi na hata nchi jirani ya Tanzania kufuatia uvamizi wa mara kwa mara uliowaletea maafa.

Akizungumza baada ya uzinduzi huo, Waziri wa Ardhi Tashrifa Bakari, amesema ari ya mstahiki Gavana Issa Timamy, nikuona kuwa mji huo umekuwa na watu wake wamerudi nyumbani baada ya kuwa wakimbizi wa ndani na kuhama makwao mnamo mwaka 1963.

Wanasimabae wamempongeza Gavana Timamy kwa kuweka historia ya kuwapimia Ardhi ambayo wazazi wao waliziacha kwa kuhama bila khiyari.

Kijiji cha Simambae kitapata sura mpya baada ya zoezi hilo la kupima mji na mashamba kukamilika.

Wakati huo huo, wakaazi wa Mkokoni walipata fursa ya Kupitia na kuidurusu ramani ya sehemu hiyo ambayo waliweza kuafikiana na upimaji kuanza mara moja.