Timu ya Kizingitini imenyakua kombe la Talanta Hela kwa chipukizi chini ya umri wa miaka 19 kwenye fainali ya kukata na shoka iliyogaragazwa katika Uga wa Shule ya Bright Star Wadi ya Shella jioni ya leo.

Kizingitini ilinyakuwa kombe hilo kwa kuwaadhibu FC Barcelona mabao mawili kwa moja.

Kaunti ya Lamu inatumia mashindano haya kutengeneza kikosi imara kitakachowakilisha Lamu katika mashindano ya kitaifa ya Talanta Hela-19.

Akihutubia halaiki akiwa ameandamana na Naibu Gavana Raphael Munywa, Gavana Issa Timamy amesema, watasubiri ripoti ya wakufunzi wawili wa zamani waliokuja kuchagua wachezaji 40 watakaochuana katika ngazi ya mkoa wa pwani kwa mchujo kabla ya kufuzu kwa finali yatakayochezwa Siku kuu ya Jamhuri kule Nairobi.

Aidha, Gavana Timamy amesema lengo la michuwano hii,ni kuhubiri amani , uwezeshaji wa kiuchumi pamoja na kubaini vipaji kwa vijana.

Timu itakayochaguliwa itatiwa kambini wakati wa likizo ya Agusti kwa ajili ya mazoezi.

Wakati huo huo, Gavana Timamy, aliwapongeza vijana kwa kuonyesha nidhamu ya hali ya juu na kuwatuza mshindi wa kwanza shilingi laki moja huku wapili akipokea elfu 50 ikiwa ni nyongeza ya zawadi kutoka mfukoni mwake.

Waliohudhuria tamasha hilo, ni pamoja na Katibu wa wafanyikazi Balozi Ali Abbas, Afisa mkuu wa wafanyikazi Abdulnasir Issa, Mawaziri wakiongozwa na Waziri wa michezo Sabastian Owanga, wawakilishi wa wa Bunge la Kaunti miongoni mwa wengine.

-Mwisho-

Kwa habari zaidi wasiliana na ofisi ya mawasiliano

kupitia communications@lamu.go.ke