Wizara ya Elimu, Vijana, Jinsia na Michezo Kaunti ya Lamu, hii leo imendaa kungamano la Uwezeshaji wa wanawake kiuchumi.

Kungamano hilo, limehudhuriwa na Mshauri wa Rais kwenye maswala ya kinamama, Bi Harriet Chiggai.

Miongoni mwa changamoto zilizojadiliwa ni:-

Dhulma za kijinsia kwa wanawake na watoto.

– Yanayoathiri wanawake kiafya.

– Hali ngumu ya kufanya biashara.

– Ndoa za mapema.

– wazazi kuficha maovu, miongoni mwa mengine.

Akihutubia wanawake hao,Bi. Chiggei ameahidi kusaidia shirika la utetzi dhidi ya Dhulma za kijinisia hapa Lamu, ili kupiga jeki harakati zao za kukabiliana na maovu hayo.

Waliohudhuria kungamano hilo ni pamoja na Waziri wa Elimu, Sebastian Owanga pamoja na Afisa wake Mkuu Madam Hafswa Difini, afisa wa Jinsia Penina Mathieu miongoni mwa wengine.