Sera na Sheria bora ni jambo msingi katika kuendesha na kufikia ufanisi katika utoaji wa Huduma za Afya

Mstahiki Gavana Issa Timamy mapema leo , ametia saini kuwa sheria miswada 2 ya Afya:- ukiwemo ule wa Sheria ya Ufadhili wa Uboreshaji wa Vituo vya Afya ya mwaka 2023 Na Sheria ya Huduma za Afya na Afya ya Jamii ya Kaunti ya Lamu ya mwaka 2023.

Sheria hizi 2 zitatoa uhifadhi na upatikanaji wa rasilimali za kutosha katika mfumo wa mapato, kwa vituo vya afya katika Kaunti ya Lamu.

Sheria hii inatoa fursa ya Mapato yanayotokana na NHIF na makusanyo ya fedha taslimu yatumike kununua bidhaa na vifaa, huku ikihakiki miundo thabiti ya kuhakikisha uendelevu na uimarishaji wa huduma za afya katika ngazi ya jamii.

Walioshuhudia hafla hiyo ya utiaji sahihi, ni Waziri wa Afya Daktari Mbarak Bahjaj, Katibu wa Kaunti Balozi, Ali Abbas, Kiongozi wa Wengi Muhishimwa Bwana Bwana, Waziri wa Uchumi wa Baharini Faiz Fankupi, Waziri wa Utalii Aish Miraj miongoni mwa viongozi wengine wa kaunti.

“TimamyCare” Afya Mashinani Afya Majumbani.