Mstahiki Gavana Issa Timamy amezindua rasmi mpango wa kadi ya bima ya matibabu NHIF kwa familia elfu 20 kwa wakaazi wa kaunti ya Lamu.
Bima hiyo ya kupokea matibabu bila malipo inagharamiwa na serekali ya kaunti ya Lamu.
Akihutubia katika hafla hiyo, Timamy amesema ikifikia mwaka ujao wa kifedha ataongeza idadi ya familia watakaofaidi na mpango huo hadi elfu 25.
Kadi hiyo ya bima ya NHIF inasimamia mzee wa boma, mke na watoto wake.
Aidha, Gavana Timamy amezindua upya kitengo cha huduma za dharura kitakachokabiliana na majanga pamoja usafirishaji wa wagonjwa ili kupata matibabu ya ziada.
Kitengo hicho kimepigwa jeki baada ya magari ya kubeba wagonjwa yaliyoharibika kwa mda mrefu kutengenezwa.
Mpango huo, unajumuisha wauuguzi na madereva ambao wamepokea mafunzo ya kukabiliana na majanga.