Serekali ya Kaunti ya Lamu kupitia Idara ya Ardhi mapema hii leo, imeandaa vikao vya Ushiriki wa umma na wakaazi wa Mokowe na Kisiwani Amu ili kukusanya maoni ya kutathmini na kudurusu kiwango cha reti zinazotozwa mashamba.

Vikao hivyo, vinanuiwa kuwajulisha wananchi umuhimu wa tathmini hiyo na ni vipi itamsaidia mlipa reti kujua kuongezeka kwa thamani ya shamba lake na kuchangia ongezeko la ushuru kwa Kaunti.

Maoni hayo, yanakusanywa kutoka miji ya Kisiwa Cha Amu, Mokowe, Hindi na Mpeketoni.

Kwa mujibu wa kifungu cha Sheria cha 267 kutoka Serekali ya kitaifa inatakiwa kufanyika kwa tathmini ya mashamba kila baada ya miaka 10.

Miongoni mwa waliohudhuria vikao hivyo ni pamoja na Waziri wa Ardhi Tashrifa Bakari, Afisa Wake Mkuu Ahmed Loo, Meneja wa Manisipaa ya Lamu Abduswamad Ali miongoni mwa wengine.

-Mwisho-

Kwa maelezo zaidi wasiliaana na afisi ya mawasiliano kwa:- communications@lamu.go.ke