Kinga ni Bora kuliko kutibu

Serekali ya Kaunti ya Lamu kupitia Idara ya Afya imezindua rasmi mpango wakukabiliana na magonjwa ya kuharisha na ugonjwa wa malaria ikiwa ni njia moja wapo ya kujitayarisha ili kupambana na makali ya mvua ya elnino inayotarajiwa kunyesha hivi karibuni.

Akizindua rasmi mpango huo kwa wakaazi wa Mokowe katika makao makuu ya afisi za kaunti, Gavana Issa Timamy amesema Serekali yake imeweka mikakati kabambe ili kuhakikisha kuwa wakaazi wake wako na afya mzuri na salama.

Aidha, Gavana Timamy amewasihi wakaazi wa wote wa kaunti ya Lamu kutojenga katika maeneo ya mapito ya maji na kuongeza kuwa huenda wakalazimika kubomoa nyumba ambazo zimejengwa juu ya njia za maji huku akitoa mfano wa eneo la Mokowe ambapo nyumba kadhaa zilisombwa na maji.

Kati ya mwezi Aprili na Julai Idara ya Afya imenakili visa 6,600 vya magonjwa ya kuharisha inayoletwa na maji machafu ya kusimama.

Vifaa hivyo ni pamoja na machine za kisasa zakupulizia dawa ya kuuwa mbu, neti za mbu pamoja na dawa za kuweka kwa maji yakunywa.

Waliohudhuria hafla hiyo fupi ni pamoja na afisa Mkuu wa wafanyikazi Abdulnasir Issa, Waziri wa Afya Dkt. Mbarak Bahajaj, wakurugenzi wa Afya pamoja na wafanyikazi wengine.

-Mwisho-

Kwa maelezo zaidi wasiliaana na afisi ya mawasiliano kwa:- communications@lamu.go.ke